Hatimaye video ya Naseeb Abdul aka Diamond Platnumz imekidhi viwango na kutambulishwa katika TV kubwa za kimataifa ikiwemo TRACE, na kuwa video ya nne ya Bongo kuchezwa na kituo hicho cha Ufaransa.
Platnumz ambaye mwezi huu ameongeza wigo mkubwa wa mashabiki wa Afrika kwa kutengeneza ushirikiano na wasanii wakubwa wa Nigeria, ameshare habari njema kupitia mitandao ya kijamii kuwa video ya single yake ‘My Number One’ imetambulishwa TRACE TV ya Ufaransa pamoja na SOUND CITY TV ya Nigeria.
Alishare picha (hapo chini) na kuandika “And now listed as one of the #New videos on TRACE #AdoadoTunaondoka #InshaAllahTutafika #WCB #Wasafi for Ever Darling”
Katika picha hiyo aliandika “Few minutes ago on Sound City Tv #TrendingVideoRequests …. #TaratibuTutafika #WCB #Wasafi for Ever Darling” Kabla ya ‘My Number 1′ ya Diamond, video pekee za wasanii wa bongo ambazo tayari zimepata nafasi ya kuoneshwa na Trace ni pamoja na ‘Party Zone’ na ‘Money’ za AY, pamoja na ‘Bila Kukunja Goti’ ya Mwanza FA na AY.
Source: Bongo5
No comments:
Post a Comment