VERSE 1:
Nilipotoka mbali na ninaheshimu nilipo/
sikuwa na umuhimu kihivyo… stimu zikanipa
elimu ya Biko/ Kimaandiko… kimistari.. hadi
fans wanascream nikirap../ sikuamini kama
nina zali mpaka nilipoidream hiphop/
Wanapagawa…. Na baadhi ya mambo
nayoyajua.. pia nina uwezo wa kufanya
mpaka madawa yanaugua/
Wanapagawa na nyimbo ngumu hawa
#teamMabiiitoz /
Achana na power window.. sijui rimz za
dimpoz/
haileti bingo, mshiko? Star ishi simple/ sanaa
iko hivyo sometimes.. hukataa kukaaa ulipo/
wanaodharau.. hujiletea matatizo..hawajui
kama wadau… hupendelea kukuona hivyo?/
bonge la staa.. donge la njaa.. hauna kitu/
jikombe ugongwe…mtaaa ukuone hauna
ishu/
ukishindwa kujiandaa… jiandae kushindwa/
mjinga utaachwa unashangaa kumuona
Martin Kadinda/
Usmati anaotinga, majumba mandinga ya
bwana Almasi.. je hizi track za harakati ni
ujinga?/
HAPANA…. nguvu ya mamba ni maji/ na
umaarufu au kutamba.. kushika namba ni
bahati..sio kipaji kama Kubanda eti
unachana kigumu/ kisa track ikivuma sana
kwenye chati haidumu /
Amani kwa chachage na MAKUWADI wa
SOKO HURIA../ baba asante kwa UTAFITI na
ZAWADI ya ALMASI ya BANDIA/NYUMBANI…
nasikiliza DUNIA YA SASA ya MARIJANI../
najiuliza tutarithi nini ikiwa IMANI
ishakwisha tangu zamani?/ labda kubisha na
wakinitisha najihami../ inasikitisha
unapoibiwa na aliyekupigisha ni jirani/
‘’Pole MAPROSOO’’ ( uhujumu –uchumi )
umefanya umetubu.. / WAZEE ni wahuni hadi
soo waay back before SUGU/
Taifa la kondoo.. huendeshwa na serikali ya
Dubu/ na MBWA MWITU wenye siri.. ili
bepari umuabudu/ kimahakama, kiserikali,
kidini umsujudu../ huo ni utumwa pia/
Unafanya vijana wanaumia../
Tunaishia kufia mabatani kama nzi ndani ya
glass ya bia..
CHORUS: ( Juma Nature )
Siri ya mtungi aijuaye kata../ komaa… kaza..
kisha utapata/ x 2
Siri ya mchezo naijua mimi.. tu.. na hakuna
mwingine x 2
VERSE 2:
Tofauti ya BIASHARA na SIASA ikila hasara
inaweza buma/ wakati SIASA kila mara ukiwa
unang’ara ujue kuna.. kinara/ anayeunda
msafara wa wanaojituma na kuchuma kwa
kukufanya uwe imara hapo hasara hakuna/
KIDUMU CHAMA CHA MASELA… Ukoloni
mambo leo umetupa uhuru wa bendera,/
tuone kufuru za wenye hela/
TANZANIA ni ‘ demu wa mtungo ‘
wanamuiita CHA WOOTE/’’ HANGOVER ..
‘’anaikimbia kwa kupiga ‘ “ mtungi “ saa
zote /Mkubwa anazuga atasolve… matatizo
ya nchi yake/ ‘’na gari bovu..’’ halisukumwi
kwa kukaa ndani yake/
MAENDELEO ni ile ndoto..MWEZEKAJI
ashaipuuza../ je Kukaa karibu na moto ni
kuuota au kujiunguza? /
hakuna UHURU wa kweli (Africa)
msidanganywe na illusion/
na daily tunafeli sababu ya POLITICAL
institutions/
CIVILIZATION imeadvance sasa wanatuua
economically../
hakuna utumwa mbaya kama ule wa kujiona
uko free/
Kuusaka ukweli ni sawa na kumenya
kitunguu/
kila ganda litakutoa machozi na utabaki
macho juu/
Ukishafika kwenye kiini niambie nini
utagundua..?
zaidi ya mafaili yaliyounganika utaghairi
kuyafunua?
Wamejivisha U-NOAH.. SAFINA zao
zikatoboka/
Wakajivisha U-MUSSA.. FIMBO zao
hazikugeuka NYOKA/
Sasa wanaujaribu U-MUNGU MTU kuamua
nani leo
atatoka….!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!???????????????????
No comments:
Post a Comment